Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu
yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale
wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya,
ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza
gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia
naye ni mwigizaji, ameelezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa
mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.
Baba
mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John
alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi
anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka
Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha anaendelea na kusema siku ya pili
yake John alimpigia simu na kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii
vizuri, kuona hivyo, baba yake mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta
amelala kwenye kochi anatoka jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?,
John akamjibu, tumbo linamuuma sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake
mzazi nimwambie tumpeleke Hospital Mwananyamala.
Tulipofika pale
hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari wakaamua wampige X
Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu makali sana tumboni
mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari, wakasema ana
matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji wa haraka.
Stephano
aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi na baba
yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za kupumulia
zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa
matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye
gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
Baada ya kufika
Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura (emergence room), na
baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye tunafaamiana naye na
kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi kufanyiwa upasuaji
kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo walidhani kuna
utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia
sehemu ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo
vipimo vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye
tumbo ndiyo maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.
Baada
ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu wa
tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na
kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi
turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi
nilifika Muhimbili na kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku
wa jana yake. Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha
kinachoendelea. Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu
yule daktari ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani
anamshughulikia hivyo alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza
punguza makali ya sumu iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip
ya maji lakini inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.
Muda
mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena,
amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake. Mazishi
yamepangwa kufanyika makaburi ya kinondoni kesho. Alisema baba mdogo wa
muigizaji Stephano.
Bongo5 Tutaendelea kukupa update kadri tutakavyozipata.
No comments:
Post a Comment