Saturday, January 19, 2013

HUYU NDO MSANII ALIYEJITOA MTANASHATI, NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA KUHUSU USTADHI JUMA NA MUSOMA


MSANII wa muziki Tanzania maarufu kama Amazon, ameamua kuweka wazi kuwa amejitoa Mtanashati Entertainment, kwa kile alichodai kuwa boss wa kundi hilo Ustadhi Juma na Musoma, alikuwa anataka kumpa mkataba wa milele, kitu ambacho kimemfanya Amazon aone ni lengo la kummaliza kimuziki.

Msanii huyo alizungumza na mwandishi wa DarTalk, na kusema kuwa kujitoa kwake ni kwa roho safi lakini amesikitishwa na boss huyo kutaka kumpa mkataba wa milele ambao utambana yeye kutofanya kazi nyingine.

Alisema kuwa kutokana na hilo atafanya muziki kivyake hadi pale atakapopata meneja mpya wa kuweza kusimamia kazi zake.

“Mimi siwezi kukaa sehemu kwa mkataba wa milele, hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya nijitoe pale naamini nitasimama kama mwanaume katika hili na nitafanya muziki wangu,” alisema.

No comments:

Post a Comment