Saturday, January 19, 2013

MWUIMBAJI WA TAARAB AKIRI KWENDA KWA WAGANGA..

 RahmaMachuppa akifanya makamuzi yake jukwaani..

Muimbaji taarab wa chama kubwa Bongo Jahazi Modern Taarab bibie Rahma Machuppa hivi karibuni alikiri kwenda kwa waganga.
Muimbaji huyo ambae anatamba na kibao chake cha 'Nipe Stara' kilichopo kwenye albam mpya ya Jahazi aliongea huku akiwa na komfidensi zote alikiri kwenda kwa waganga mara kwa mara kwa ajili ya kuweka nyota yake sawa na kujitoa nuksi na mikosi lakini sio kwa lengo la kumroga mtu.
Mwanadada huyo mwenye makeke na makomfinfidence ya ajabu awapo jukwaani alizidi kufunguka katika kituo kimoja cha televisheni na kusema hata akiambiwa na mganga akavunje 'nazi' mchana kweupe mbele ya adhala ya watu atafanya ilimradi mambo yake yamnyookee. Pia alitoa ONYO KALI kwa yoyote ataeenda kumroga kwani lolote litalompata asije akaenda kumuomba msamaha maana hatokuwa tayari KUMSAMEHE KABISAA!!!
Haya wadada wa kibongo mnaoendaga kuroga alafu mnakataa kabisa kuwa amuamini mambo ya ushirikina MPOO!! Maana wengine mmejaa chale mwili mzima alafu bado mwajifanya amuamini uchawi tuwaeleweje?? Wengine tunawajua mnakeshaga kwa waganga HADI MKAKOSWAKOSWA KUOLEWA NA WAGANGA alafu mnatudanganya amuamini ushirikina ndio nini!! Ebu kuweni na moyo wa ujasiri kama Rahma jamani na sio kujifichaficha wakati ndio vinara wa kukesha makaburini kuroga.
MNAJIJUWA!!
Mi nimemaliza kama una la zaidi toa comment apo tujue..

sOURCE: ZEddylicious

No comments:

Post a Comment