Wednesday, January 23, 2013

MUONEKANO MPYA WA WIZ KHALIFA NA WATOTO WAKE

USIKOSE JUMAPILI HII PALE MAISHA CLUB - MABESTE NIGHT

JUMAPILI HII NDANI YA MAISHA CLUB USIKOSE USIKU WA MABESTE NIGHT

MAGARI YAHARIBIWA VIBAYA BAADA YA UKUTA KUANGUKA UBUNGO



.
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani na nje ya nchi cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amesema, idadi ya magari yaliyoangukiwa yanakadiriwa kufikia 24.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela

ZIARA YA MH.RAIS JK NCHINI UFARANSA



c2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo.
PICHA NA IKULU
c3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini hum.
c6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika maongezi rasmi na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa na ujumbe wake  katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L’Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013
c7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L’Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013
c9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L’Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013
c11
Gari iliyomchukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiondoka Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L’Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013(picha na Ikulu)

KESI YA LULU:WANASHERIA KUOMBA DHAMANA

Msanii wa Filamu za kibongo Elizabeth Michael alias Lulu baada ya kipindi cha nyuma kurudishwa rumande kwa kesi yake inayomkabili kwa kutuhumiwa kumuua msanii mwenzake,The Late  Steven Kanumba,sasa taarifa ambayo tumeipata ni kwamba wanasheria wake ambao ni Peter kibatala na Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe wametuma maombi ya dhamana ya kesi ya Lulu ili isomwe haraka kwasababu muombaji amekaa muda mrefu mahabusu.
Wanasheria hao baada ya kuwasilisha maombi hayo katika mahakama Kuu wanatarajia kesi hiyo kusikilzwa tena siku ya tarehe 25 mwazi huu mbele ya Jaji Zainabu Mruke.

JACK CLIFF NA JUX VUITTON WAZUA MANENO BAADA YA KUTUMA PICHA KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM

 Kama utakuwa unamfahamu mwanadada Jack Cliff ambaye ameshawahi kushirikishi katika video mbili kama Queen Video ambazo ni Nataka Kulewa na she got a gwan ya Ngwair na nyinginezo,
sasa mrembo huyu baada ku post picha hii katika mtandao wa instagram watu wengi sana wanauliza na maswali mengi juu ya Jux na Jack Cliff huko China.
Huku Jux kupitia katika akaunti yake ya instagram alipost picha hiyo hapo juu ambayo jack Cliff akijaribisha kuvaa viatu vyake na kuandika Baby Tryn them #me Jordan...#dope though.

SHAA KUTOKA NA NGOMA MPYA TAREHE 28 MWEZI HUU

Shaa baada ya ukimya katika muziki wa Bongo Fleva sasa mwaka huu amejipanga vema na ameweka wazi kupitia katika mtandao wa instagram, kwamba siku ya tarehe 28 mwezi huu anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "Promise" na akaamua kuweka cover mpya ya ngoma hiyo.
Wale mashabiki wa Shaa Kaa tayari kwa ujio huo mpya kutoka kwa msanii huyo soon kutoka.

NISHER:NASHUKURU MUNGU NIMEMALIZA KUTENGENEZA VIDEO MPYA"PRESS PLAY"

Baada ya kuwasili hapa Dar kwa ajili ya kutengeneza video mpya ya Dj choka kutoka B hits inayofahamika kwa jina la Press Play,sasa leo kupitia katika akaunti ya Nisher aliandika ujumbe na kusema kwamba wamemaliza jana ku shooting video mpya ya "Press play"

Huu ndiyo ujumbe kutoka katika ukurasa wake wa Facebook

HII NDIYO NGOMA MPYA YA IZZO BUSNESS FT QUICK ROCKA,NGWAIR "BALL PLAYER"

FAHAMU KUHUSU,TAMKO LA MWISHO LA BEN PAUL KUHUSU KOLABO,WIMBO MPYA YA IZZO BIZNESS,KURUDI KWA G UNIT.


Kama unakumbuka vizuri mwaka jana Ben Paul alisitisha kufanya Collabo na msaani yoyote mpaka February 3, 2013, Lakini hapa katikati tumeskia Yatakwisha ft Linnah, Lord Eyes ft Ben Paul - No More Drama na Mama Yoyo Aliyoshirikishwa na G Nako. Leo Ben Paul ametengua kaulia yake kuhusu kusitisha kufanya collabo na kusema atakuwa akifanya collabo kwenye Ngoma nzuri .Ataangalia Potential ya Msanii ,Wimbo wenyewe na Production. Ben alisema ata International artist wanafanya collabo nyingi ila hawashuki kwa sababu wanazingatia Mambo hayo.

Kuhusu wimbo wake wa kwanza kutoka mwaka huu Ben amesema `Jikubali' Inamuhusu mtu anaye Weka Tofauti kati yake na watu wenye mafanikio, watu maarufu na ata wanasiasa. Hii ngoma itamuhamasisha afanye vizuri kwenye jambo analolifanya ,kama ni kazi , elimu ,sanaa au chochote. Huu wimbo unampa nafasi yakujiona ni mtu mwenye uwezo wakufanya kazi nzuri na akafanikiwa na kusaidi familia yake. Mtu huyo atuone sisi kama watu wa kawaida. Wimbo unatoka Kupitia Video kwanza alafu audio ndio itafata.
Hamisa ,Izzo Bizness Na Sammisago
Rapper Izzo Bizness amesema Ball Player Inaanza Audio na ni mara ya kwanza kufanya wimbo na watu watatu.Izzo amesema ameamua kubadilisha style kidogo kwani ingekuw marudio ya mwaka jana .Wimbo unatoka kesho na WaTanzania ndio wataamua kama ni ujio mzuri wa Izzo au Akajipange tena .Kwenye wimbo huu ataskika kwa mara ya Kwanza Msanii Ruth aliyefanya Chorus. 
Manager wa Rapper Game amesema yupo kwenye mchakato wa kurudisha kundi la G-Unit kama wasanii, 50 Cent na Game wata weka tofauti zao pembeni na kutengeneza pesa kwa pamoja .
Fahamu Ni takribani miaka kumi toka umemuona 50 Cent na Game waki share mic na Manager Dontay "Taydoe" Kidd amesema  50 Cent anajua hakuna G Unit bila game na Game anajua G Unit haiwezi kufanya vizuri bila yeye kwa sasa.Dontay anategemea kutengeneza pesa nyingi kama G Unit litarudi tena kufanya kazi pamoja kwani walikuwa na mashabiki sana . Dontay alisema wakirudiana tu atahamisha jitiada zake kwenye bidha za G Unit kama T Shirt , viatu ,kofia , na mpaka simu za G Unit.

HIVI NDIVYO SIKU YA KUTEMBEA NA CHUPI ILIVYOSHEREKEWA DUNIANI KOTE

HII NDO SEHEMU MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST JOHN ALIPOKUTWA KAUAWA

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliekuwa anasoma nurse amekutwa amefariki katika njia iendayo chuoni hapo, taarifa za awali zinasema kuwa alikuwa anakuja kujisomea chuoni hapo mida ya usiku, inaonekana alikutana na watu wabaya wakati anakuja kujisomea na kumbaka maana nguo zake zilikutwa pembeni ya mwili wake, vilevile mwili wa marehemu huyo ulikuwa umeliwa mnyama inasemekana fisi.



Hapa polisi wakiuchukua mwili wa marehemu huyo





Hapa polisi wanauweka mwili wa marehemu huyo kwenye gari, endelea kutufatilia kwa taarifa zaidi tutazidi wajulisheni.

FID Q ATUNUKIWA CHETI MAALUMU NA "UNDER THE SAME SUN"



Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma Under The Same Sun kwa mchango wake mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Ngosha amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika hilo la Canada,Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi yanayosomeka "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)."

Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.

baada ya miezi kadhaa walirudi tena kanda ya ziwa kuwarudishia shukurani wakaazi wa kanda ya ziwa kwa sababu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yalipungua sana hivyo kampeni yao kwa kushirikiana na wakaazi wa kanda ya ziwa ilifanikiwa.

HATIMAYE SHAKIRA NA MUMEWE WAPATA MTOTO WA KIUME

http://sandrarose.com/images17/shakira-baby-bump.jpg?42e305 
Nyota wa Pop wa nchini Colombia, Shakira amejifungua mtoto wa kiume jana mjini Barcelona, Hispania.Shakira ametoa taarifa hizo kupitia website yake ambayo iliandikwa kwa Kiingereza, Spanish na CatalĂĄn:
“We are happy to announce the birth of Milan PiquĂ© Mebarak, son of Shakira Mebarak and Gerard PiquĂ©, born January 22nd at 9:36pm, in Barcelona, Spain.The name Milan (pronounced MEE-lahn), means dear, loving and gracious in Slavic; in Ancient Roman, eager and laborious; and in Sanskrit, unification.”
Baba wa mtoto huyo ni mchezaji wa FC Barcelona, Gerard Piqué.

ANGALIA JINSI ASKARI MWANZA, WALIVYOTEMBEZA KIPIGO KWA WAENDESHA BODABODA






Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia - FFU mkoani Mwanza jana asubuhi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi, risasi za moto pamoja na kutembeza mkong'oto kwa waendesha pikipiki, maarufu kama bodaboda wa jiji la Mwanza ambao walikuwa wakipambana na askari wa kikosi cha usalama barabarani wakipinga kukamatwa kwa pikipiki zao, katika operesheni iliyoendeshwa na jeshi la polisi mkoani humo.

ASKARI WA JWTZ AKAMATWA NA PEMBE ZA NDOVU


JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kwamba mwanajeshi aliyekamatwa juzi katika tukio la ujangili mkoani Arusha ni askari wake. Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe jana alimtaja askari huyo kuwa ni mwenye namba MT 59509 Sajenti, Azizi Athuman Yusufu ambaye alisema ni askari wa jeshi hilo na alikuwa dereva wa mkufunzi wa kijeshi kutoka Zimbabwe anayefundisha hapa nchini.

Hata hivyo Kanali Mgawe alisema mkufunzi huyo wa kijeshi, hakuwapo wakati wa tukio hilo. “Kweli huyo ni askari wetu. Alikuwa anamwendesha mkufunzi wa
kijeshi kutoka Zimbabwe. Siku hiyo alimrudisha nyumbani kwake saa saba mchana na kwenda kupaki gari. Lakini baadaye saa moja usiku, alikwenda kulichukua gari hilo na kutokomea nalo kusikojulikana hadi alipokutwa katika tukio hilo,” alisema Kanali Mgawe.

Wakati JWTZ likitoa taarifa hiyo, Polisi mkoani Arusha jana lilieleza jinsi askari huyo alivyokamatwa. Hata hivyo namba ya askari huyo ilitofautiana na namba ya askari ikimtaja kuwa ni mwenye namba MT 59503.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema askari huyo alikamatwa saa 5:00 usiku wa Januari 20 mwaka huu. Alikutwa na pembe mbili za ndovu na bunduki moja aina ya Riffle yenye namba 458.

“Tunaamini bunduki hiyo ndiyo iliyotumika kwenye uwindaji huo haramu,” alisema.

Kamanda Sabas alidai kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na wenzake zaidi ya wawili ambao walikimbia wakati mwenzao huyo anakamatwa eneo la Manyara Kibaoni Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

“Gari lililohusika kwenye uhalifu huu limethibitika kuwa ni mali ya JWTZ na uchunguzi unaendelea kujua namna gani wahusika walifanikiwa kuondoka nalo kambini na kwenda kulitumia kwenye uhalifu huo,” alisema Sabas.

Awali, habari kutoka eneo la tukio zimeeleza kuwa gari hilo lilikuwa na zaidi ya abiria watatu ambao mara baada ya matairi mawili kupasuka, moja la mbele kulia na jingine la nyuma kushoto watu wawili waliteremka na kutokomea porini na mizigo isiyojulikana.

Ilidaiwa kuwa baada ya wananchi kufika kwa nia ya kutoa msaada kwa majeruhi, mtuhumiwa aliyekutwa akiwa amevaa jaketi la JWTZ na suruali ya jinsi pamoja na bunduki, aliwahakikishia wananchi waliotaka kuwakimbiza watu hao wakidhani wamemwibia wasishughulike nao kwa kuwa hajaibiwa chochote.

Baada ya wananchi na askari wa jeshi la polisi waliofika kumtilia shaka mtuhumiwa, msako ulifanyika kuelekea walikokimbilia abiria hao garini na mizigo, lakini hawakuonekana.

ANGALIA PICHA ZA MTOTO ALIEZIKWA MZIMA NA KUFUKULIWA NA KUKUTWA MZIMA

Mama mmoja nchini Nigeria ameamua kumzika mtoto wake akiwa hai. Baada ya taarifa kupatikana polisi walienda na kuamua kufukua. Baada ya kufukua walimkuta mtoto huyo na kumkimbiza hospitali aliposafishwa mtoto huyo alikutwa hai.

HIVI NDIVYO WANAFUNZI WA ST JOHN DODOMA, WALIVYOMUAGA MWANAFUNZI MWENZAO ALIYEUAWA JUZI

Marehemu mama yetu na mwanafunzi mwenzetu LYDIA LEO
Hapa wanafunzi pamoja na walimu wakijipanga kuupokea mwili wa marehemu mama yetu, mwanafunzi mwenzetu LYDIA LEO





Uzuni majonzi ndio iliyotawala moyoni mwetu kwa kumpoteza mwanafunzi mwenzetu LYDIA LEO



Wanafunzi wakiwa ukumbini kwa ibada ya kumuaga mwanafunzi mwenzetu LYDIA LEO
Sisi sote ni wake Mola na kwake tutarejea, tulimpenda sana LYDIA LEO ila mwenyezi Mungu amempenda zaidi, Bwana alitwa na bwana ametoa. Twamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen. Mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Matombo mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.