Wednesday, January 23, 2013

FAHAMU KUHUSU,TAMKO LA MWISHO LA BEN PAUL KUHUSU KOLABO,WIMBO MPYA YA IZZO BIZNESS,KURUDI KWA G UNIT.


Kama unakumbuka vizuri mwaka jana Ben Paul alisitisha kufanya Collabo na msaani yoyote mpaka February 3, 2013, Lakini hapa katikati tumeskia Yatakwisha ft Linnah, Lord Eyes ft Ben Paul - No More Drama na Mama Yoyo Aliyoshirikishwa na G Nako. Leo Ben Paul ametengua kaulia yake kuhusu kusitisha kufanya collabo na kusema atakuwa akifanya collabo kwenye Ngoma nzuri .Ataangalia Potential ya Msanii ,Wimbo wenyewe na Production. Ben alisema ata International artist wanafanya collabo nyingi ila hawashuki kwa sababu wanazingatia Mambo hayo.

Kuhusu wimbo wake wa kwanza kutoka mwaka huu Ben amesema `Jikubali' Inamuhusu mtu anaye Weka Tofauti kati yake na watu wenye mafanikio, watu maarufu na ata wanasiasa. Hii ngoma itamuhamasisha afanye vizuri kwenye jambo analolifanya ,kama ni kazi , elimu ,sanaa au chochote. Huu wimbo unampa nafasi yakujiona ni mtu mwenye uwezo wakufanya kazi nzuri na akafanikiwa na kusaidi familia yake. Mtu huyo atuone sisi kama watu wa kawaida. Wimbo unatoka Kupitia Video kwanza alafu audio ndio itafata.
Hamisa ,Izzo Bizness Na Sammisago
Rapper Izzo Bizness amesema Ball Player Inaanza Audio na ni mara ya kwanza kufanya wimbo na watu watatu.Izzo amesema ameamua kubadilisha style kidogo kwani ingekuw marudio ya mwaka jana .Wimbo unatoka kesho na WaTanzania ndio wataamua kama ni ujio mzuri wa Izzo au Akajipange tena .Kwenye wimbo huu ataskika kwa mara ya Kwanza Msanii Ruth aliyefanya Chorus. 
Manager wa Rapper Game amesema yupo kwenye mchakato wa kurudisha kundi la G-Unit kama wasanii, 50 Cent na Game wata weka tofauti zao pembeni na kutengeneza pesa kwa pamoja .
Fahamu Ni takribani miaka kumi toka umemuona 50 Cent na Game waki share mic na Manager Dontay "Taydoe" Kidd amesema  50 Cent anajua hakuna G Unit bila game na Game anajua G Unit haiwezi kufanya vizuri bila yeye kwa sasa.Dontay anategemea kutengeneza pesa nyingi kama G Unit litarudi tena kufanya kazi pamoja kwani walikuwa na mashabiki sana . Dontay alisema wakirudiana tu atahamisha jitiada zake kwenye bidha za G Unit kama T Shirt , viatu ,kofia , na mpaka simu za G Unit.

No comments:

Post a Comment