Wednesday, January 16, 2013

EMMANUEL OKWI AUZWA KWA DOLA LAKI 3 ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA

Sakata la mchezaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman limefikia mwisho.

Kwa taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya $300,000.

Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi karibuni.

"Ni kweli Mwenyekiti yupo Tunisia akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel. Ada ya uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache ujao dili litakamilika na Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi binafsi na klabu yake mpya." - kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba.

Etoile du Sahel ni klabu mojawapo yenye mafanikio makubwa barani Afrika, ikiwa inashikilia rekodi ya kuwa klabu pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na CAF.

Kwa taarifa zaidi kuhusu ukamilikaji wa dili hili endelea kutembelea tovuti hii.
CHANZO: SHAFI DAUDA

No comments:

Post a Comment