Sunday, January 20, 2013

MABAO 3 DHIDI YA MABAO 2 NDIYO YALIIPA YANGA USHINDI JANA ILIPOCHEZA NA BLACK LEOPARD

Wachezaji wa Young Africans wakisalimiana na wachezaji wa Black Leopard kabla ya kuanza kwa mchezo
Mabingwa wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati almaarufu kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club imeifunga timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaaam.
Young Africans iliyokuwa nje ya nchi kwa kambi ya mafunzo takribani wiki ilikuwa ikicheza mbele ya washabiki wake, iliweza kucheza soka safi na la kuvutia kipindi chote cha mchezo huku Black Leopard ikipata wakati mgumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Didider Kavumbagu alikosa bao la wazi dakika ya 21 ya mchezo akiwa yeye na mlinda mlango wa Black Leopard Ayanda Mtshali, lakini shuti alilopiga lilipaa juu ya lango la timu hiyo.
Yanga iliednelea kuutawala mchezo kwa wachezaji wake kupigiana migongeo mizuri na kuutawala mchezo hasa eneo la kiungo, Kabange Twite alishindwa pi akuipatia Yanga bao katika dakika ya 25 baada ya kushinda kumalizia pasi safi ya Mbuyu Twite.
Dakika ya 32 Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Balck Leopard Harry Nyirenda kumuangusha Haruna Niyonzima katika eneo la hatari, amabpo mwamuzi Hashim aliamuru upigwe mkwaju wa penati na Jerson Tegete kuukwamisha mpira huo wavuni.
Yanga iliongeza kasi ya kusaka bao la pili lakini shambulizi liliofanywa na Mbuyu Twite liliokolewa na mlinda mlango wa Black Leopard Matshal kabla ya Mbuyu tena kupiga kichwa kilichopaa mita chahce juu ya lango la timu ya Black Leopard.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Young Africans 1 – 0 Black Leopard.
Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo kocha Brandts aliwatoa Kabange Twite, Mbuyu Twite na golikipa Ally Mustafa ‘Barthez’ nafasi zao zikachukuliwa na Juma Abdul, Saimon Msuva na golikipa Said Mohamed.
Dakika ya 47, Humphrey Khoza aliipatia Black Leopard bao la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Edagr Manaka kufutia kutokuwepo kwa mawasilaino kati ya mlinzi Nadir Haroub na mkinda mlango wake Said Mohamed.
Kiungo chipukizi Frank Domayo aliipatia Young Africans bao la pili dakika ya 63 ya mchezo, akimaliza pasi safi iliyopigwa na kiungo Haruna Niyonzima na mpira huo kumkuta Domayo ambaye alimchambua mlinda mlango wa Black Leopard Mtishal na kuhesabu bao la pili.
Dakika 10 baadaye mshambuliaji Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la tatu kwa umakini akimalizia pasi ya kungo mshambuliaji Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa timu ya Black Leopard na kumpasia mfungaji aliyeukwamisha mpira huo wavuni.
Jerson Tegete nusra angeipatia Young Africans bao la nne, kufuatia lakini krosi iliyopigwa na Saimon Msuva kuokolewa na mlinzi wa Black Leopard sentimeta chache pemebeni mwa lango huku Tegete tayari akiwa tayari kwa kuukwamisha mpira huo.
Dakika ya 89, Black Leopard ilijipatia bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mshambuliaji wake Rodney Magalela kufuatia mlinzi wa kulia wa Young Africans kumcheza madhambi mshambuliaji huyo katika eneo la hatari.
Mpaka mpira unamalizika Young Africans 3- 2 Black Leopard.
Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kwa kupata ushindi huo wa leo, kwani timu ya Black Leopard ni timu nzuri, imecheza vizuri lakini mwisho wa siku vijana wangu walikuwa ni bora zaidi ndio maana wameibuk ana ushindi huo.
Kambi yetu ya mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa kujiamini wametulia hawana presha ya mchezo, hali inayopelekea kucheza migongeano kwa uhakika na hii ni dalili tosha kuwa tupo tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom alisema ‘Brandts’
Young Africans: 1.Ally Mustapha ‘Barthez’/Said Mohamed, 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub’Cannavaro’, 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd ‘Chuji’, 7.Kabange Twite/Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Didier Kavumbagu/Said Bahanuzi, 10.Jerson Tegete/George, 11.Haruna Niyonzima
Black Leopard: 1.Ayanda Mtshali, 2.Ernort Dzaga, 3.Nkosiyabo Xakane, 4.Harry Nyirenda, 5.Humphrey Khosa, 6.Munganga Djunga Jean, 7.Mongezi Bobe, 8.Thomas Madimba, 9.Abbas Amidm, 10.Edagr Manaka 11.Rodney Ramagalela

No comments:

Post a Comment