Tuesday, August 13, 2013

Ebhana eeeh hiki ni kioja zaidi ya kioja,mastaa hawa
 kutoka majuu kila kukicha ukisikia ili
kesho watakuja na ili sio kiubaya lakini laasha ni katika
kuweka maisha yao halisia na kuonesha
kile ufanyaga wanapokuwa nyumbani kwa mashabiki zao....
Msanii Nicki Minaj mwenye asili ya visiwa vya
Trinidad & Tobago siku ya jana kupitia
mtandao wake wa Instagram aliweza kuweka
picha hizi na kuonesha sehemu
ya mwili wake tena akimanisha ni maziwa yake
 kiujumla yakionekana wazi kabisa...
Mwanadada huyo mwenye mvuto wa aina yake kama
 ilikuwa aitoshi aliweka picha nyingine
na kuandikia maneno "#Titythursday a day to celebrate"....
Kumbe alikuwa anafanya vile kama kuonesha ishara
 ya kusherekea siku ya matiti duniani so
kama mwanamke aliamua kuweka vile
kuonesha kufurahia siku hiyo......
Naona umejionea mwenyewe hapo au sio
 basi usikose kupitia hapa kwenye
Blogsite hii kupata habari moto moto za ndani na nje
 ya nchi kiburudani,michezo na kitaifa....

Picha: Mmiliki wa Home Shopping Center akiwa South Africa kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali



MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko  Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hali yake inadaiwa kuendelea vizuri, lakini kuna uwezekano wa jicho lake moja kutokuona kabisa baada ya kuathirika sana, lakini jicho la pili liko salama.
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.

Baada ya kuachia "Salamu Zao" wenye salamu washamtuma Ney Salam zao


Ikiwa ni siku chache tu mara baada ya kuachia single yake mpya "Salamu zao" Ney wa mitego amepokea salamu zake kwa ujumbe mfupi kutoka kwa mmoja wa  aliekuwa kwenye kamati ya mazishi ya marehem Albert Mangweha "Ngwea" .

Meseji hizo ambazo Ney hakutaja ni nani exactly aliezituma, zinaonyesha kumuuliza Ney kama hiyo ni hiphop au nini maana ni kama kuwatukana.
Baada ya kupost picha hiyo yenye meseji hizo, Ney aliandika kuwa meseji ziko nyingi na ataendelea kuzipost  na wala haogopi vitisho vyao na kuwaomba wanakamati hao kupeleka pesa zilizokuwa zimepatikana katika mazishi ya Ngwea kwa mama yake mzazi hata kama nikimya kimya maana bado muda wanao 


Kwenye wimbo huo wa salamu zao Ney ametuma salamu zake pia kwa Mh Zitto Kabwe na kumtaka aachane na bongo fleva maana hawamtaki, Kigoma all stars imemshinda, Madam Rittah pia salamu zake kuhusu BSS pia zipo huko na kuuliza mill 50 zinaenda wapi maana wasanii wao wamechoka na wengine kibao.....

CHIDI BENZI AMEKIRI KUA ALKA ANATUMIA MADAWA YA KULEVYA KWA MUDA MREFU NA SASA AMEAMUA KUACHA..ALISEMA LEO HII AKAIWA KWENYE INTERVIEW YA NYIMBO YAKE MPYA ....


Rapper Chidi Benz amekiri kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu, na baada ya kuzidiwa nayo ameamua kuachana nayo na kupatiwa matibabu Nairobi, Kenya.
Chidi amekiri leo hii kupitia kipindi cha XXL pale alipofika kwa ajili ya kuachia wimbo wake mpya ambao amewaachia mashabiki kuupa jina lake.
hidi alianza kufunguka mara baada ya kuulizwa na Lachico kuhusu ngoma hii ambayo imefanyika ndani ya wiki moja wakati alikuwa kimya mda ina maana alikuwa harikodi au?

Chidi Benzi: ngoma nimefanya nyingi sana, zingine nimetoa lakini zilikuwa hazina nguvu sana kwasababu usimamiaji ulikuwa chini na kipindi kile kulikuwa kuna mambo mengine ambayo tulikuwa tunahusika nayo yanakuchanganya akili unakuwa unafikiria mawazo mengi lakini usambazi tu na wewe mwenyewe kujiweka kikazi nilikuwa siko hivyo.

Lachico: Ulikuwa unawaza nini ambayo ilikuwa inakuchanganya akili? 

Chidi Benzi: eeeh mambo mambo tu mavitu mengi unajua binaadam unakua unakutana na vitu unaonana navyo unaungana na vitu unapishana navyo, kwahiyo vitu vitu tu.

Lachico: Ok kama unafikiri kwamba inaweza kutusaidia kushare na sisi au kama ni ersonal tunakuruhusu uiweke iwe personal?.
Chidi Benzi: Aaah naweza kushare kwasababu tu familia iliniambia nisizungumzie sana  ila naweza nikashare kwasababu nilikifanya na nikaamua watu wote wapate hisia kuwa Chidi amefanya, ofcourse nilikua najihusisha na vitu vingi ambavyo ni vilevi na nini, nilikuwa nikitumia vitu vingi sana kwahiyo utumizi ule ulikuwa unanifanya saa zingine nakuwa na hasira na mawazo mengine tofauti tofauti, namchukia kila mtu na nini, kwasababu natumia vitu mbavyo vinavyozidi, naweza tukaongea na wewe lachico hivi story lakini nitoka pale  namwambia lachico snich tu yaani unakuwa na anger unakuwa na hasira, kwahiyo sasa dakika ya mwisho nikagundua naficha watu au naamua kwenda kufanya kitu kwaajili ya afya yangu na maisha yangu.

Lachico: Mimi namaindi kujua ni vilevi vya aina gani ambavyo unavizungumzia hapa?

Chidi Benz: aaah pombe, ganja madawa na vinginevyo vinginevyo

Lachico: kwahiyo unataka kuniambia pamoja na kwenda Nairobi pia ulikuwa umekwenda rihab pia.

Chidi: No sikua rihab ndo maana huwa sitaki kuizungumzia wala kupost kwenye ma website na nini, lakini ni kama nilienda then baada ya kufika nikakutana na Nonini kutoka airport tu gari linaanza kwenda nikagundua kwanza sikufatilia kama ulikuwa ni muda wa baridi kwahiyo nikagundua kuna baridi, then jamaa anaanza kuniambia yooo unajua tuna show kama saba, nane tisa kumi, kumi na mbili, nikamwambia show ngapi? umeniambia show kama tatu tu, akasema eeh nilikuwa nataka tu uje tunashow kama 7 nane yaani show nyingi, utaweza au unadhani kuna vitu ambavyo utavihitaji ambavyo itakuwa ngumu kwako?

 nikamwambia yaaah kuna vitu nitavihitaji, mimi bana kuna vitu navyovitumia nimefikia nikikaa twenty minutes bila hivyo vitu ni noma yaani ni noma nachanganyikiwa nakuwa akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje.akaniambia Chidi na mimi unanijua, unajua yeye nikama anakunywa pombe lakini siku mojamoja sasa unajua mi ntapaje Chidi na nairobi ni gharama,
 nikamwambia ok, nikamwambia lakini pia nnawazo lingine kuna mtu alinitonya kuwa kunakitu ambacho kinaweza kufanyika ni pensa nyingi kama milioni 15 , 16 hivi za kibongo, kama kikifanyika hicho basi nanyofolewa kabisa hivyo ambavyo vilikuwa vinanifanya niwe hivyo, akaniambia hiyo naijua lakini ni process ndio maana dunia nzima hawafanyi hiyo unaskia watu wanakufa daily na madawa hawafanyagi hiyo wewe je? 
nikamwambia mi nafanya kwasababu sasa nishakutana na vitu vingi kama ni maumivu, ni ishu aibu nishakuta nazo za mapenzi za maisha kawaida ntashindwa kufanya hicho, akaniambia watu huwa wanakufa sometimes ikikuzidia, nikamwambia ntafanya si kuna hospitali ni dawa nitafanya.
hela ikapatikana nakumbuka tuka arrange, daktari kaja kanitibia fresh, kwahiyo mi sijaenda rihab wala sijatumia methadon sijui maana zile ni mradi tu.

Lachico: ulitibiwa kwa njia gani?

ni dawa ambayo inanunliwa na unachomwa kama mgonjwa tu, yenyewe inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inaenda kukaa, then baada ya dakika kadhaa pakikauka panakua pakavu, ni kama ile sehem inakua ni mbichi ukivuta, lakini ukiwa huna hela huvuti panakuwa pakavu pakikauka ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuwa na alosto, lakini kama ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea, so yenyewe inaenda ni kama mapovu, panasafisha panakuwa empty ni wewe mwenyewe uamue uendelea kuvuta ama uache kabisa, lakini yenyewe inakusafisha pale kote, unaanza kuwa na power, inakupa akili, uso, rangi ya uso, mwili unaanza kubadilika, unaanza kuwa fine.,,,,,,,so niko fresh, niko healthy, nakula naishi vizuri naskia vizuri na nime-calm down.