Friday, February 1, 2013

WAKILI WA ‘LULU’ ASIKITISHWA NA WASANII WA BONGO MOVIE KWA KUTOKUWA NA USHIRIKIANO

SIKU chache baada ya kuachiwa kwa dhamani kwa kesi inayomkabili ya kudaiwa kuua bila kukusudia msanii wa filamu Elizabeth Machael ‘Lulu’, wakili wake Peter Kibatala, amesema kuwa amesikishwa na kitendo cha wasanii wa tasnia hiyo kushindwa kujitokeza mahakamani siku zote za kesi hiyo na hata siku ya mwisho ambayo wamepewa dhamani.

Wakili huyo akizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa kitendo cha wasanii kutojitokeza mahakamani siku zote za kesi au siku ya mwisho ambayo Lulu alikuwa anapewa dhamana kunatia shaka kwamba ndani ya tasnia hiyo hakuna upendo na huwa wanapendana kwenye raha pekee.

Alisema kuwa mbali na hao lakini amekuwa na furaha kwa kiasi kikubwa kutokana na upendo uliokuwepo kutoka kwa wasanii Dr Cheni na Monalisa ambao wamekuwa karibu na familia ya Lulu hadi siku ya dhamana ambapo ndiyo waliompokea mahakamani.

No comments:

Post a Comment