Monday, March 18, 2013

WHY 90% YA MAMIS BONGO HAWAOLEKI? WAJUE WAREMBO HAO HAPA

WAKATI mashindano ya u-miss yanaanzishwa Bongo, wazazi wengi walikuwa wazito kuwaruhusu watoto wao kushiriki wakiamini kwamba ni uhuni. Kadiri miaka ilivyozidi kusonga mbele, taratibu walianza kuelewa kuwa siyo uhuni na wakawaruhusu watoto wao kwa kuyaona yana tija.
Flaviana Matata.
Matunda ya warembo yalionekana, lakini kumekuwa na dosari kwao, licha ya mafanikio makubwa wanayoyapata, asilimia kubwa hawaolewi. Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini hawaoleki, why?
Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema, sababu inayosababisha warembo hawa wasiolewe au hata wakiolewa wasidumu kwenye ndoa ni jinsi wenyewe walivyojijenga akilini kuwa ni watu maarufu, wazuri hivyo wamekuwa wakichagua wanaume na kuishia kutumiwa, wakija kushtuka umri unakuwa umewatupa.
Ifuatayo ni orodha ya warembo ambao wamepitia kwenye mashindano mbalimbali ya u-miss lakini mpaka sasa hawajaolewa na wengine wameishia kuzalishwa tu:

WEMA SEPETU
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ni mzuri na kila mwanaume rijali akimuona lazima amkubali. Wema alishikilia Taji la Miss Tanzania mwaka 2006 lakini mpaka sasa hajaolewa na amewahi kuvishwa pete za uchumba mara kadhaa lakini ndoa imempiga chenga.
SYLIVIA SHALLY
Miss Ilala mwaka 2009/10 kila mmoja alivutiwa na uzuri wake, ameishia kuzalishwa ambapo baba wa mtoto wake hajulikani.
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Ni mrefu, mrembo na mzuri. Kabula alishikilia Taji la Miss Kariakoo miaka ya nyuma lakini pamoja na uzuri wake, ameishia kuzalishwa na prodyuza, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ na baada ya hapo mapenzi yaliisha na hakuna mpango wowote wa ndoa kati yao.
JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Huyu alishikilia Taji la Miss Upanga mwaka 2005, hajaolewa. Anaendesha laifu lake kupitia uigizaji, hana dalili za kuolewa, naye amezalishwa.
ISABELA MPANDA
Huyu ni Miss Ruvuma 2006, ameingia kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva baada ya mashindano kuisha. Bado hajaolewa, alivishwa pete ya uchumba na kutolewa mahari lakini aliishia kuzaa na sasa ana watoto wawili. Ndoa kwake bado ni kitendawili.
MIRIAM JERALD
Ni Miss Tanzania mwaka 2010. Alitangaza uchumba wake na msanii wa filamu Kennedy ‘Kenny’ na kuahidi kuwa watafunga ndoa mwaka jana lakini ahadi hiyo haijatimia na ameishia kuzalishwa.
RASHIDA WANJARA
Alishikilia Taji la Miss Mara mwaka 2000 ni mrembo na umri umekwenda lakini hadi sasa hajaolewa na hajawahi kuzungumzia suala la ndoa.
JOKATE MWEGELO
Ni mrembo aliyeshikilia Taji la Miss Tanzania namba 2, mwaka 2006. Mwanadada huyu mpaka sasa hajaolewa na aliwahi kutajwa kuwa mpenzi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
SALHA ISRAEL
Huyu ni Miss Tanzania mwaka 2011. Ni mrembo lakini bado hajaolewa na ishu zake za kimapenzi hazijulikani.
FLAVIANA MATATA
Ni mrembo aliyeshikilia Taji la Miss Universe 2007/08 lakini mpaka sasa hajaolewa na anatusua masuala ya urembo katika anga za Kimataifa.

No comments:

Post a Comment