Historia mpya inakaribia kuandikwa duniani baada ya mwanaume ambaye
anajulikana kwa jina Andrew Wardle, kutoka Stalybridge, Greater Manchester huko
Uingereza ambaye alizaliwa bila uume, kufanya mpango wa kutengenezewa na
kuwekewa kiungo hicho kwa njia ya oparesheni.
|
Andrew
Wardle |
Mwanaume huyu ambaye kwa sasa anaumri wa
miaka 39, anatarajiwa kuwa mwanaume wa kwanza kabisa duniani kufanyiwa
oparesheni kama hii na ajabu zaidi ni kwamba, kiungo hiki kitatengenezwa kutoka
sehemu ya mkono wake.
|
Andrew
Wardle |
Katika mahojiano yake na mtandao wa The
Sun, Wardle mwenyewe anasema kuwa, hakuwahi kufikiria kutokea kwa siku ambayo
anaweza kupata kiungo hiki muhimu kwa mwanaume na ambacho kinafanya kazi
sawasawa, na endapo itakuwa ni ya mafanikio, ataanza kuishi kama mtu wa
kawaida.Madaktari kutoka chuo kikuuu cha
London tayari wameshakiri ugumu wa zoezi ili lakini wamesema kuna uwezekano
mkubwa wa kufanikiwa.
Katika hali yake aliyokuwa nayo sasa, Wardle anadai
kuwa amekwishawahi kulala na zaidi ya wanawake 100, na asilimia 20% tu ya
wanawake hawa ndio alioweza kuwaambia ukweli.
Wardle kwa sasa anafanya
kazi kama mlinzi, mpishi na mhudumu na katika historia yake, amekwishapata
matukio mbalimbali ya kunyanyaswa kutokana na hali yake na kupoteza marafiki
kadhaa wa kike, na amekwishakuwa akijihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya
kama kitu cha kumfariji.
No comments:
Post a Comment