Monday, December 30, 2013

HUDDAH MONROE WA KENYA AMPIGA DONGO JACK CLIFF KWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Aliyekuwa muwakilishi wa Kenya kwenye
shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’,
Huddah Monroe aka Thee Boss Lady amerusha
dongo kwa mrembo wa Tanzania Jackie Cliff
ambaye alikamatwa na dawa za kulevya aina
ya Heroin nchini china.
Tweet ya Huddah inadai kuwa Jackie Cliff ni
mrembo ambaye alitaka kuishi maisha mazuri
ya haraka na kutumia vitu vya kifahari, pia
akaambatanisha na picha mbili
zinazomuonesha Jackie akiwa amepozi kabla ya
kukamatwa na nyingine akiwa na pingu, picha
iliyotolewa na gazeti la nchini China.
Katika tweet nyingine Huddah ambaye hupenda
kuonesha maisha ya kifahari anayoishi,
amefunguka zaidi na kuonesha kuwa yeye ni
muoga na asingeweza kufikia kiwango hicho.
“So this beautiful Tanzanian girl was caught
with a KG of Cocaine. That’s now a BAD ASS
B**CH! I’m such a coward…I swear I’m not
BAD!” Huddah ametweet.

No comments:

Post a Comment