Tuesday, August 13, 2013

CHIDI BENZI AMEKIRI KUA ALKA ANATUMIA MADAWA YA KULEVYA KWA MUDA MREFU NA SASA AMEAMUA KUACHA..ALISEMA LEO HII AKAIWA KWENYE INTERVIEW YA NYIMBO YAKE MPYA ....


Rapper Chidi Benz amekiri kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu, na baada ya kuzidiwa nayo ameamua kuachana nayo na kupatiwa matibabu Nairobi, Kenya.
Chidi amekiri leo hii kupitia kipindi cha XXL pale alipofika kwa ajili ya kuachia wimbo wake mpya ambao amewaachia mashabiki kuupa jina lake.
hidi alianza kufunguka mara baada ya kuulizwa na Lachico kuhusu ngoma hii ambayo imefanyika ndani ya wiki moja wakati alikuwa kimya mda ina maana alikuwa harikodi au?

Chidi Benzi: ngoma nimefanya nyingi sana, zingine nimetoa lakini zilikuwa hazina nguvu sana kwasababu usimamiaji ulikuwa chini na kipindi kile kulikuwa kuna mambo mengine ambayo tulikuwa tunahusika nayo yanakuchanganya akili unakuwa unafikiria mawazo mengi lakini usambazi tu na wewe mwenyewe kujiweka kikazi nilikuwa siko hivyo.

Lachico: Ulikuwa unawaza nini ambayo ilikuwa inakuchanganya akili? 

Chidi Benzi: eeeh mambo mambo tu mavitu mengi unajua binaadam unakua unakutana na vitu unaonana navyo unaungana na vitu unapishana navyo, kwahiyo vitu vitu tu.

Lachico: Ok kama unafikiri kwamba inaweza kutusaidia kushare na sisi au kama ni ersonal tunakuruhusu uiweke iwe personal?.
Chidi Benzi: Aaah naweza kushare kwasababu tu familia iliniambia nisizungumzie sana  ila naweza nikashare kwasababu nilikifanya na nikaamua watu wote wapate hisia kuwa Chidi amefanya, ofcourse nilikua najihusisha na vitu vingi ambavyo ni vilevi na nini, nilikuwa nikitumia vitu vingi sana kwahiyo utumizi ule ulikuwa unanifanya saa zingine nakuwa na hasira na mawazo mengine tofauti tofauti, namchukia kila mtu na nini, kwasababu natumia vitu mbavyo vinavyozidi, naweza tukaongea na wewe lachico hivi story lakini nitoka pale  namwambia lachico snich tu yaani unakuwa na anger unakuwa na hasira, kwahiyo sasa dakika ya mwisho nikagundua naficha watu au naamua kwenda kufanya kitu kwaajili ya afya yangu na maisha yangu.

Lachico: Mimi namaindi kujua ni vilevi vya aina gani ambavyo unavizungumzia hapa?

Chidi Benz: aaah pombe, ganja madawa na vinginevyo vinginevyo

Lachico: kwahiyo unataka kuniambia pamoja na kwenda Nairobi pia ulikuwa umekwenda rihab pia.

Chidi: No sikua rihab ndo maana huwa sitaki kuizungumzia wala kupost kwenye ma website na nini, lakini ni kama nilienda then baada ya kufika nikakutana na Nonini kutoka airport tu gari linaanza kwenda nikagundua kwanza sikufatilia kama ulikuwa ni muda wa baridi kwahiyo nikagundua kuna baridi, then jamaa anaanza kuniambia yooo unajua tuna show kama saba, nane tisa kumi, kumi na mbili, nikamwambia show ngapi? umeniambia show kama tatu tu, akasema eeh nilikuwa nataka tu uje tunashow kama 7 nane yaani show nyingi, utaweza au unadhani kuna vitu ambavyo utavihitaji ambavyo itakuwa ngumu kwako?

 nikamwambia yaaah kuna vitu nitavihitaji, mimi bana kuna vitu navyovitumia nimefikia nikikaa twenty minutes bila hivyo vitu ni noma yaani ni noma nachanganyikiwa nakuwa akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje.akaniambia Chidi na mimi unanijua, unajua yeye nikama anakunywa pombe lakini siku mojamoja sasa unajua mi ntapaje Chidi na nairobi ni gharama,
 nikamwambia ok, nikamwambia lakini pia nnawazo lingine kuna mtu alinitonya kuwa kunakitu ambacho kinaweza kufanyika ni pensa nyingi kama milioni 15 , 16 hivi za kibongo, kama kikifanyika hicho basi nanyofolewa kabisa hivyo ambavyo vilikuwa vinanifanya niwe hivyo, akaniambia hiyo naijua lakini ni process ndio maana dunia nzima hawafanyi hiyo unaskia watu wanakufa daily na madawa hawafanyagi hiyo wewe je? 
nikamwambia mi nafanya kwasababu sasa nishakutana na vitu vingi kama ni maumivu, ni ishu aibu nishakuta nazo za mapenzi za maisha kawaida ntashindwa kufanya hicho, akaniambia watu huwa wanakufa sometimes ikikuzidia, nikamwambia ntafanya si kuna hospitali ni dawa nitafanya.
hela ikapatikana nakumbuka tuka arrange, daktari kaja kanitibia fresh, kwahiyo mi sijaenda rihab wala sijatumia methadon sijui maana zile ni mradi tu.

Lachico: ulitibiwa kwa njia gani?

ni dawa ambayo inanunliwa na unachomwa kama mgonjwa tu, yenyewe inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inaenda kukaa, then baada ya dakika kadhaa pakikauka panakua pakavu, ni kama ile sehem inakua ni mbichi ukivuta, lakini ukiwa huna hela huvuti panakuwa pakavu pakikauka ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuwa na alosto, lakini kama ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea, so yenyewe inaenda ni kama mapovu, panasafisha panakuwa empty ni wewe mwenyewe uamue uendelea kuvuta ama uache kabisa, lakini yenyewe inakusafisha pale kote, unaanza kuwa na power, inakupa akili, uso, rangi ya uso, mwili unaanza kubadilika, unaanza kuwa fine.,,,,,,,so niko fresh, niko healthy, nakula naishi vizuri naskia vizuri na nime-calm down.

No comments:

Post a Comment