Tuesday, August 13, 2013

Baada ya kuachia "Salamu Zao" wenye salamu washamtuma Ney Salam zao


Ikiwa ni siku chache tu mara baada ya kuachia single yake mpya "Salamu zao" Ney wa mitego amepokea salamu zake kwa ujumbe mfupi kutoka kwa mmoja wa  aliekuwa kwenye kamati ya mazishi ya marehem Albert Mangweha "Ngwea" .

Meseji hizo ambazo Ney hakutaja ni nani exactly aliezituma, zinaonyesha kumuuliza Ney kama hiyo ni hiphop au nini maana ni kama kuwatukana.
Baada ya kupost picha hiyo yenye meseji hizo, Ney aliandika kuwa meseji ziko nyingi na ataendelea kuzipost  na wala haogopi vitisho vyao na kuwaomba wanakamati hao kupeleka pesa zilizokuwa zimepatikana katika mazishi ya Ngwea kwa mama yake mzazi hata kama nikimya kimya maana bado muda wanao 


Kwenye wimbo huo wa salamu zao Ney ametuma salamu zake pia kwa Mh Zitto Kabwe na kumtaka aachane na bongo fleva maana hawamtaki, Kigoma all stars imemshinda, Madam Rittah pia salamu zake kuhusu BSS pia zipo huko na kuuliza mill 50 zinaenda wapi maana wasanii wao wamechoka na wengine kibao.....

No comments:

Post a Comment