50 Cent pia amesema kuwa, kutokana na mabadiliko ambayo yamekuwa yakitokea hapa katikati katika Studio ya Interscope ambayo ndiyo imekuwa inasimamia mpango huu, ikiwepo watu wanaofanya kazi katika studio hii kubadilika, ameona ni bora kusubiri mpaka mambo yatakapotulia kabisa, kauli ambayo inaashiria kuwa kunamuda mrefu hapa katikati mpaka mzigo wa Street king Immortal kukamilika na kutoka.
Studio Albam ya mwisho ya 50 Cent ni ile ya mwaka 2009 - Before I self Destruct, na baada ya hapo ameachia mixtape kadhaa kabla ya kutoa albam ambayo pia haikuwa ni kwa madhumuni ya kibiashara - Murder by Numbers.

Msanii huyu kwa sasa, Nnje ya muziki na biashara yake kubwa ya Energy Drinks [Street King to be specific] kati ya nyinginezo nyingi, pia amejiingiza katika field nyingine za burudani ikiwepo TV na pia upromota wa mapambano ya Ndondi.
No comments:
Post a Comment