Monday, July 15, 2013

CHEKI HAPA MJI MZURI KULIKO YOTE DUNIANI NA VYANZO VYAKE....

Kama utakuwa na kumbukumbu basi moja ya makala ambazo
nimekuandalia huu ni mwendelezo wake...
Makala ya Jinsi Dubai ilivyokuwa hadi leo walivyowekeza
na vitega uchumi,nikiwa nimekuonesha sehemu
mojawapo za vitega uchumi vya nchi hii ya falme za kiarabu......

Picha hizi utakazoziona hapa ni picha halisia za maendeleo ya nchi
hiyo mojawapo unaweza kujionea
jinsi mfano wa Mti wa Mnazi na Matawi yake lakini hapa unajionea
mti huo ukiwekwa baharini ukitengenezwa
kwa kusukuma maji na kujenga makazi ya watu na hoteli za kitalii..
Kama ulikuwa hujui basi acha nikujuze hapa,kwa sasa Dubai ndio
Mji mzuri kupita miji yoyote duniani
kutokana na vitega uchumi kama hivi,ni ajabu kuona au kufikiria
kufanya kitu kama hiki,cha kwanza yahitaji moyo
cha pili yahitaji ushirikiano na moja ya hela zilizotumika ni
kodi za wananchi na hela ya serikali....
Hii inatokanaje.......? Je wajua?? Serikali yenye watendaji
Imara na Uadilifu wanaweza kufanikisha mambo kama haya
kuzuia ufujaji wa hela na rushwa huku Dubai rushwa ni adui namba
moja na kutokana na sheria ya nchini humo
ukipokea rushwa ni kuhukumiwa kunyongwa........
Hali kama hiyo inatisha hadi viongozi na kuamua kujitolea
kufanya kazi kwa hali na mali
kufikia kuwaletea maendeleo wananchi wake.....
Picha hii ni mwonekano wa kaskazini wa mfano wa mti wa
mnazi uliotengenezwa nchini dubai
ndani ya bahari,unaweza kuona majengo marefu na hata
 njia mbalimbali za magari....
Picha halisia ya kile nilichokuelezea kwa juu hapa unaweza kuiona saawia kabisa....
Kusini mwa Mti huu unaweza kuona sehemu hii shuguli mbalimbali zinafanyika...

Picha ya Juu kabisa unaweza kuona mandhari ya kitu nachokuelezea
na kuvuta taswira ya kile nilichokujuza
pale juu....
Hiki ni kitu kingine kabisa.....Angalia picha hii kwa umakini
 utatambua kitu kama mimi nachokuambia,
ni ramani ya dunia ikiwa imetengenezwa mita 10,000 kutoka usawa
wa nchi kavu wa bahari nchini
dubai.....Unaweza kuona kitu hiki ni cha ajabu kabisa lakini ni
kweli kipo kabisa na kama unavyshuudia wewe
mwenyewe....
Mfano wa mti wa Mnazi unavyoonekana kwa usiku wakati wa
 ufunguzi wa sehemu hiyo iliyotengenezwa
na mafundi na Wakandarasi waliobobea kutoka nchini Uholanzi kwa
 muda wa miaka 4 kujenga kitu
hiki na imegharimu zaidi ya dolla Bil.8 za kimarekani kufanikisha ujenzi huu....
Angalia mandhari ya eneo ili lililojengwa kwa ramani ya
 dunia na unavyoona ni makazi ya watu
wanaishi kabisa ndanio ya ya ramani hiyo ya dunia....
Mandhari zahiri ya Sehemu husika pembezoni mwa ramani
ile ukiona sehemu za pembeni ni nyumba na
hoteli za kitalii ....!!                     









No comments:

Post a Comment