Friday, January 17, 2014

Picha: LILE BEEF KATI YA WASANII WA MUZIKI H:BABA NA DIAMOND PLATNUMZ LAISHA

Akizungumza na Blogger wetu jana, H.Baba aka Baba
Tanzanite alisema katika kusherehekea siku hiyo
muhimu ameona ni vyema asawazishe makosa
yote yaliyotokea nyuma ili awe mpya.
“H.Baba ni mpya sihitaji beef sasa hivi nahitaji
kufanya kazi. Diamond namheshimu na yeye
ananiheshimu,kama nilimkosea mimi au
alinikoea mimi tusameheane,sisi ni binadamu
nimeona niyamalize ili tuishi kwa amani,”
amesema muimbaji huyo.
“Tokea sakata la wizi wa nyimbo lilipotokea
sema tulikuta na tukazungumza,lakini mimi
imebidi niwe wa kwanza kusema kwamba hili
jambo liishe kabisa. Nilizaliwa sina beef na mtu
kwahiyo Nasib Abdul naomba tusameheane toka
moyoni na pia kama kuna yoyote nilikosa naye
naomba tusameane.”

Wednesday, January 1, 2014

Picha: Samsung yazindua TV kubwa zaidi duniani, ni ya inch 102, inauzwa milioni 240

TV hiyo imeingizwa sokoni kwa mara ya kwanza
Korea Kusini ikiwa inauzwa 160million won ya
Korea Kusini sawa na shilingi milioni 241 za
Tanzania.
TV hiyo inatumia teknolojia ya U-HDTV (Ultra-
High Definition Television) inayosababisha picha
kuonekana vizuri zaidi ya mara nne ya TV za HD
za kawaida.