Monday, April 29, 2013

CHECK OUT OICHA 3 ZIKIMUONYESHA CHEGGE AKIWA ZAKE SWEDEN ...

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

PADRI AFUMANIWA NA MKE WA MTU! STORY NA PICHA KAMILI HIZI HAPA

KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.

MSHANGAO: Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
MSAMAHA: Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe (jina tunalo) alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”
NI IBILISI TU: Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.
AWEKWA KITIMOTO
Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.
Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.
Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!
AIBU: Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.
SIKU ZA NYUMA
Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.
Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema  zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.
Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
CHUKUA SURUALI YAKO PADRE: Father Ngowi akipatiwa suruali yake.
IJUMAA WIKIENDA NA FATHER NGOWI SASA
Baada ya kujazwa madai hayo, kama ilivyo desturi ya Magazeti ya Global Publishers likiwemo hili (Ijumaa Wikienda), lilimsaka Father Ngowi kwa udi na uvumba ambapo Ijumaa iliyopita nyakati za mchana lilifanikiwa kuzungumza naye lakini kabla ya kufanya hivyo, kifaa cha kunasia sauti kiliwekwa sawa na mambo yalikuwa hivi:
Wikienda: Haloo, naongea na Father Ngowi wa Parokia ya Korongoni, Marangu, Moshi?
Father Ngowi: Naam ni mimi, nani mwenzangu?
Wikienda: Naitwa…(mhariri anataja jina), napiga simu kutoka Magazeti ya Global Publishers.
Father Ngowi: Uko wapi?
Wikienda: Makao Makuu ya Global Publishers, Dar es Salaam.
Father Ngowi: Eeh…unasemaje?
Wikienda: Kuna madai ya wewe kukutwa na mke wa mtu chumbani. Je, unaweza kunielezea kama ni kweli na tukio lilikuwaje?
Father Ngowi: Siyo mimi.
Wikienda: Wewe siyo Father Urbanus Ngowi?
Father Ngowi: Nimekwambia siyo mimi, hao ni matapeli wanataka pesa ndiyo wametengeneza hizo picha.
Wikienda: Kwa hiyo unataka kuniambia hizi picha ni za kutengeneza?
Father Ngowi: Nimekwambia hao ni matapeli wanataka pesa.
Wikienda: Ulishaziona picha zenyewe?
Father Ngowi: Sijui.
NGOMA YATUPWA KWA MKUU WA JIMBO
Wikienda: Mbona tayari tukio hilo linadaiwa limeshafika kwenye ngazi ya jimbo, Moshi kwa Father Paul Uria?
Father Ngowi: Muulize yeye ndiye mkubwa wangu.
Wikienda: Basi nisaidie namba yake ya simu ya mkononi.
 
Father Ngowi akiwa katika vazi la kipadre.
Baada ya takribani dakika 10, Father Ngowi alituma namba ya simu ya Father Uria na mambo yakawa hivi:
Wikienda (huku kinasa sauti kikiendelea kufanya kazi): Haloo…naitwa …(mhariri anajitambulisha) kutoka Magazeti ya Global Publishers, Dar es Salaam, naongea na Mkuu wa Jimbo Kanisa Katoliki, Moshi, Father Uria?
Father Uria (kwa sauti yenye unyenyekevu): Ndiyo.
Wikienda: Una taarifa za mtumishi wako, Father Ngowi kunaswa na mke wa mtu chumbani?
Father Uria: Kwanza mimi si mkuu wa jimbo, ni mwakilishi wa mkuu wa jimbo. Sipo mjini kwa sasa nipo Kilema huku vijijini kwenye huduma lakini nilikuta ‘missed calls’ zake jana (Alhamisi) kwani ilikuwa tukutane kwa sababu alishanijulisha kuwa kuna tukio kama hilo unaloniambia wewe.
NGOMA YAWA NZITO, YATUPWA LEO JUMATATU
“Kweli tulikuwa tukae jana lakini ikashindikana, leo (Ijumaa) ni sikukuu (Muungano), kesho (Jumamosi) na keshokutwa (Jumapili) ni wikiendi. Kwa hiyo tutakaa Jumatatu (leo) hivyo nipigie saa 10:00 jioni siku hiyo ili nikupe maagizo tutakayofikia na mengine.
Wikienda: Lakini Father Ngowi alikueleza tukio lilikuwaje?
Father Uria: Nimekwambia tukikaa ndiyo tutajua kilichotokea. Wewe nipigie hiyo saa 10 nikupe kitakachojiri.
Wikienda: Shukrani Father Uria kwa ushirikiano.
Kazi haikuishia hapo, Ijumaa Wikienda lilimgeukia tena Father Ngowi walau aseme kwa ufupi kilichomtokea.

CHECK OUT PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA SHOW YA DIAMOND UINGEREZA


PICHA: KWA WALE MASHABIKI WA MPIRA WA KIKAPO INAWAHUSU SANA HII ONA JINSI HARUSU YA MCHEZA MPIRA WA KIKAPU MICHAEL JORDAN ILIVOKUA..

Hapa Walikuwa Pamoja Mwaka 2011.






PICHA TOFAUTI ZIKIMUONESHA DIAMOND AKIWA KWENYE JIJI LA MALKIA ELIZABETH


  
               Hapa msanii Diamond Platnumz akiwa ameshapata breakfast yake na Dancers wake katika mjii wa malkia elzabeth .........             

     
                    Hapa akiwa na moja ya dancr wake mose iyobo katika bus......  

  
    Hapa wakiwa washakula.... na washashiba pembeni....... ni DUmi utamu ,                     mose iyobe bila kumkosa Rais wao Diamond ...........


Wednesday, April 17, 2013

NDOTO YA LINEX YAKAMILIKA KWA WYREE

Msanii Linex leo hii amekamilisha ndoto yake ya siku nyingi kufanya kazi na msanii maarufu kutoka Kenya "Wyre", ngoma hiyo ambayo kwa msaada wa digitali inaelekea kukamilika, imetengenezwa beat na producer Fundi Samweli ambae yupo Sweden kwa hivi sasa, ambayo ilitumwa kwa Linex na kuipeleka kwa producer Mswaki ambae pia ameongezea maujuzi yake, na hapo ndipo linex akaingiza sauti zake.
Hatimae leo beat na vocal za Linex zimetumwa Kenya kwa ajili ya Wyre kuingiza sauti leo usiku na kisha kuongezea maujuzi pia akiwa kama producer..kuonyesha furaha ya kukamilisha asilimia kubwa ya kazi hiyo Linex ameamua kushare na mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa facebook kwa kuandika status hii
Linex Sunday
Siku ya leo imekua nzuri sana kwangu nimepiga kazi na mtu nnaemzimiaga kitambo linex ft wyre cumn soon but sita ahidi ni lini itatoka but saiz ndo kazi imeisha God is good

MAKALA ILIYOANDIKWA SIKU CHACHE KABLA YA KIFO CHA BI KIDUDU, BI KIDUDE AKIELEZEA HISTORIA YA MAISHA YAKE

http://www.laivu.com/maraha/files/2013/04/bi-kidude-564x4231.jpg
FATMA binti Baraka, maarufu kwa jina la Bi Kidude, ni miongoni mwa wasanii wanawake wachache ambao ni magwiji wa muziki wa taarabu nchini, ambaye kwa siku ya leo ataibeba manowari yetu ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8.
Bibi huyu mwenye sauti nzito na inayopenya vyema masikioni mara anapoimba, ni mzaliwa wa Zanzibar lakini asili ya kabila lake ni Mmanyema kutoka Mkoa wa Kigoma, magharibi mwa nchi.
Licha ya kuwa na umri mkubwa (113) , sauti ya Bi Kidude bado ni nzuri na yenye kuvuta hisia, hasa kwa mpenzi wa miondoko ya muziki wa mwambao.
Bi Kidude katika nyimbo zake nyingi amekuwa akiwavutia wengi kutokana na nyimbo zake kubeba ujumbe wa mahaba kama alivyoimba kwenye wimbo wake ’Ya Laiti napenda pasi kifani’ na wakati mwingine mafumbo kwa lugha ya Kiswahili yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa watu maalumu kama alivyoimba katika wimbo wake wa ’Muhogo wa Jang’ombe’.
Hadi hapo utaona kwamba mtu mzima huyu anapaswa kupewa heshima katika siku kama hii, hasa kwa kuzingatia kwamba ni Siku ya Wanawake Duniani.
Historia na asili ya jina Kidude Fatma Baraka kwa kauli yake, anasema amezaliwa miaka 113 iliyopita huko Zanzibar ambako baba yake mzazi alilowea akitokea Kigoma (enzi za utumwa), hivyo kabila lake ni Mmanyema, tena mwenyewe anajiita ni Mmanyema asilia.
Ingawa hafahamu kijiji halisi alichozaliwa baba yake, Bi kidude anasema babu yake upande wa mama alikuwa Mngindo, wenyeji wa Kilwa.
“Mimi asili yangu ni Mmanyema wa Kigoma, baba yangu na mama yangu alikuwa Mngindo, lakini baba yangu alilowea Zanzibar, ndiyo nasisi tukazaliwa huko mpaka sasa naishi Zanzibar, lakini mie Mmanyema,” anasema Bi kidude alipozungumza na Tanzania Daima hivi karibuni.
Anasema jina la Kidude alipewa na mjomba wake wakati alipozaliwa kwa sababu alikuwa na umbile dogo. “Nimezaliwa miezi saba... njiti, nililazwa kitandani, nilikuwa mdogo, mtu hawezi kujua kama kuna kitu kimelazwa.
“Kuna mjomba wangu akaja akakaa nilipolazwa mimi, akaambiwa angalia usimkalie mtoto, akasema mtoto gani, ni kidude tu hiki, basi ndo tangu siku hiyo jina limenieleleza.
Mkongwe huyu wa taarabu nchini, ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amejizolea umaarufu kupitia tasnia hiyo, anasema katika maisha yake hajapata kuwa na mtoto, ingawa ameweka bayana kwamba aliwahi kuolewa mara mbili.
Kwa muonekano ni kikongwe mwenye nguvu zake, anasema katika umri alionao, amepitia misukosuko ya aina tofauti za maisha. Kifupi, safari yake kimaisha ni ndefu.
Anafafanua kwamba ndoa yake ya kwanza alifunga na Ramadhani Ibrahimu, na wa pili aliitwa Juma Kombo.
“Nimeolewa vyuo viwili, cha kwanza nikaachika, nimewahi kumfumania mume wangu (nadhani anamaanisha huyo wa pili), nikampiga kwa mikia ya taa nikamwacha anachuruzika damu, nikaenda zangu na mpaka leo sijaolewa na wala sina haja ya kuwa na mume,” anasema.
“Sijisifu, ila miye mpaka kesho ukiniudhi wallahi sitafuti mtu... nitawatuma watu wakuite, ukifika mie nimeandaa fimbo yangu, nikikuchapa nayo, ikimpata mtu anasimama kama anatafuta pesa,” anasema Bi kidude na kuongeza utani, jambo linalokulazimu kuendelea kumsikiliza bila kuchoka.
Anaendelea kuwausia hususan wasichana walio katika umri wa kuolewa kwamba wanaume wa sasa hivi si wema wengi wanapenda kumkuta mwanamke ana kila kitu. “Hakuna wanaume sasa hivi, hao walikuwepo zamani, siyo leo... leo mwanaume anakufuata, umlishe, umfanyie kila kitu, waapiii! Wanaume enzi hizo,” anasisitiza Bi kidude.
Maisha yake na uimbaji Mkongwe huyu wa taarabu na muziki wa mwambao nchini anainadi siri yake katika fani kuwa ni kipaji. Katika hilo Bi Kidude anasema ameanza kuimba akiwa binti wa miaka 10, alipokuwa akitoroka kwao na kwenda nyumbani kwa marehemu Mtumwa binti Saadi, maarufu Siti binti Saad.
Kadhalika, anatanabaisha kwamba mafanikio kwa mwanamuziki bora ni yule anayetumia kichwa na dhati ya moyo wake kwenye kuimba. Anasema kubana au kuibadili sauti wakati wa kuimba si sahihi, inamtoa mwimbaji kwenye uhalisia wake.
“Mie naimba kwa kutumia kichwa, si kifua au kubana pua aaa! Sifanyi kama hao wanaojiita waimba taarabu wa siku hizi, kwanza siku hizi hakuna taarabu. Mimi nina uwezo wa kuimba bila kutumia karatasi... kwani bendi ya polisi! (kicheko kwa wanaomsikiliza).
“Enzi zetu taarabu ulikuwa mtu ukiisikiliza ufanye kazi kupata maana yake kutaka kulinda matusi na kila mmoja anaweza kuisikiliza popote. Kwanza watu walikuwa wanaanza kuimba saa nane za usiku, ikifika saa 11 unafungwa muziki. Mie nashangaa siku hizi taarabu inaanza saa mbili.
“Taarabu ya zamani mtu ulikuwa ukitisa kichwa taratibu, wanawake tulikuwa tunavaa kwa heshima, si siku hizi watu mnakatika mabuno (viuno), wanawake wanakwenda bila heshima, au kwa vile kuna matako ya Kichina?” anahoji mwanamuziki huyo huku akitoa pakiti yake ya sigara aina ya Embassy na kuvuta.
Kuhusu sigara na uimbaji, Bi kidude hakubaliani na dhana kwamba inamaliza sauti, badala yake anashuhudia kwamba ameanza kuvuta akiwa kijana lakini sauti yake haina mabadiliko.
“Nimevuta sigara mie hujazaliwa na mpaka sasa navuta sijapata TB wala ugonjwa wa mapafu, leo unaniambia mbaya! Mbona sijafa?” anahoji mkongwe huyo na kueleza kwamba alianza kuvuta sigara aina ya Seven Seven, Mkasi, Simba, Kulindondo, Gundufleki na sasa Embassy ambapo ana uwezo wa kumaliza pakiti moja kwa siku tatu.
Mbali ya kuimba, pia Bi kidude ana uwezo wa kupiga ngoma, ikiwa ni baada ya kujifunza kwenye majahazi wakati akiwa na umri mdogo alipokuwa akitoroka kwenda madrasa (chuo cha elimu ya Kiislamu).
“Nilikuwa nakimbia nyumbani, naaga naenda chuo lakini sifiki, nazuga kwa kubeba juzuu yangu kwapani lakini siendi huko, bali nakwenda kwenye majahazi kufundishwa kupiga ngoma na tumba,” anasisitiza.
Oktoba mwaka 2005 alipata Tuzo ya heshima ya msanii mwenye mafanikio makubwa iliyotolewa nchini Uingereza (tuzo ya WOMAX).
Aliyebaini kipaji chake Bi Kidude, anapasua ukweli kwamba mtu wa kwanza kuthamini kazi zake na kumtafuta hadi kufika alipo alikuwa Rais mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Anasema alipokuwa Rais wa Zanzibar, aliwaomba watu wamtafute Bi Kidude ili apate kumwimbia nyimbo za Siti, kwa kuwa hakuna aliyeweza kuziba pengo japo kidogo la Siti binti Saad.
“Ali Mwinyi alikuwa akitafuta nyimbo za Siti binti Saad. Akatumwa Vuai na Khadija Baramia ambao siku nyingi hatujaonana.
“Walipotokea wakaniambia natafutwa na Ali Hassan Mwinyi, mie nikashangaa, kwa sababu nyumba zetu zilikuwa zikitizamana milango, nikaona bora niende... nikapelekwa Bwawani nikatengenezewa chumba kama kuku.
“Teena! Nikawa namwimbia Mwinyi kule Bwawani akija anaburudika... huko nikakutana na Mariam Hamdani (dada wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakhia Hamdani Meghji) alikuwa anakuja kunipiga picha anapeleka Ujerumani miye Bi Kidude sijui,” anasema.
Aidha, anafahamisha kwamba alipelekwa kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani na Mariam Hamdani, aliyemtambulisha kwa watu mbalimbali ambapo aliweza kusimama kwenye majukwaa na kutumbuiza.
Kama hiyo haitoshi, Bi kidude anaongeza kwa kusema Mariam alimpeleka hadi kwa Malkia Elizabeth II nchini Uingereza. “Yeye ndiye alinipeleka Ulaya, sikujua Kiingereza, nikawa na mlinzi, miye nimefika hadi kwa Malkia Mtukufu Lizabet (Elizabeth)... akawa ananisalimia Shikamoo mama Kidude.
“Nimepewa cheo na Mtukufu Lizabet. Nilipofika anafunua vitabu naona sura yangu nikawa nashangaa, alinipa kidani cha dhahabu nikaamua kukiuza kulekule Uingereza, maana ningekuja nacho huku wangeniua,” anasema.
Katika hilo, Bi kidude anasema alipofika kwenye kasri la malkia alikutana na askari waliofanana na sanamu, wamevalia viatu vya chuma huku akieleza kwamba hajawahi kuliona kochi kama aliloliona huko.
“Wakati natoka kwa Mtukufu Lizabet nilijikojolea ndani ya gari kwa hofu mambo niliyoyaona makubwa,” anasema Bi Kidude ambaye ni binamu wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Salmin Amour.
Akiwa nje ya Tanzania, mkongwe huyo anaeleza anavyothaminiwa huku akisisitiza kwamba Mkurugenzi wa Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Ruge Mutahaba, pia alimsaidia na kumfikisha alipo.
“Mimi, Ruge miye sikumjua huku, kanikuta napiga ngoma kwa Shakira, kanipenda akanichukua kaenda kunikodia hoteli alipojua naimba ndo akanikaribisha ofisini kwake, tunaongea ananihoji, kisha ananipa pesa anaondoka, mie nabaki hotelini tena.
“Siwi na shida miye, nakwenda ofisini kwa Ruge, simuombi mwenyewe ananigawia pesa, ananiuliza upo au haupo, namwambia narudi Unguja na yeye akija Unguja lazima afike nyumbani kwangu, anachukua alichonacho ananigawia, simuombi aah! Ananitumikia yeye. Hii ni mara ya pili anakuja kunichukua kwa ajili ya tamasha,” anasisitiza huku akimwomba Mungu ambariki mkurugenzi huyo.
Miongoni mwa nyimbo zinazompa umaarufu Bi kidude hadi sasa ni Muhogo wa Jang’ombe, Yalaiti, Kijiti, Arebaba na Machozi, Machozi ya huba na nyinginezo.
Anavyoijua Dar es Salaam Bi kidude anasema anaifahamu vilivyo Dar es Salaam kwa kuwa amefika hapa enzi za utawala wa Mwarabu wakati wazawa wakitoa kodi ya kichwa.
“Nchii hii kaitengeneza John Rupia miye niko hapa, mama Haambiliki alikuwa anafanya vichekesho, nimemlea miye, mama mzazi wa mwanamuziki Shakira nimemlea miye. Hao kina Mzee Yusuf nimewalea wazazi wao.
“Nimekuja hapa binti sijaolewa, nimekuja kwa madhumuni ya kuimba taarabu, nilifikia Bagamoyo, Rais Jakaya Kikwete, kazaliwa mikononi mwangu mie, nilikuwa naishi kwa Sheikh Ramia.
“Nimewahi kuishi Ajipshini (Egyptian) kwa miaka tisa,” anasisitiza gwiji huyo wa miondoko ya taarabu ambaye hivi karibuni alikonga nafsi ya Rais Kikwete na Watanzania waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya Mradi wa Malaria iliyokwenda kwa jina la ’Zinduka.’

WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA BAADA YA LORI KUVAMIA NYUMBA WANAYOISHI, CHEKI PICHA HAPA

Gari aina ya scania yenye nambali za usajiri T578 ALS likiwa na tela nambli T125 AGM lililobomoa nyumba na kusababisha vifo vya watu 3 wa familia moja

Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi hii ni miili ya watu waliofariki kwa kugongwa na roli hilo














Wananchi wa kijiji cha Ilongo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakiwa msibani
WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa baada Gari aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana  Usiku. Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
  
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa Tatu na Robo usiku katika Kijiji cha Ilongo Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ajali hiyo ilihusisha  magari kugongana na kugonga nyumba na kusababisha vifo na majeruhi.


Alisema chanzo cha ajali kilitokana na Gari lenye namba za usajili T578 ALS likiwa na tela lenye namba za usajili T125 AGM aina ya Scania likiendeshwa na dereva ambaye hakuweza kutambulika liligonga  kwa nyuma  gari lenye namba T959 ASC aina ya Scania.
  
Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Juhudi Saimon(34)Mnyiha mkazi wa Dar Es Salaam kisha gari hilo  kugonga nyumba mali ya Matia  Mwagala mkazi wa Kijiji cha Ilongo.
  
Aliwataja matrehemu kuwa ni Asia Yahaya (52)mkulima na Msangu, Abubakari Yahaya(8) Msangu na mwanafunzi darasa la pili  aliyekuwa anasoma katika Shule ya msingi Ilongo na Fatuma Yahaya (6) Msangu mwanafunzi wa darasa la kwanza  Shule ya Msingi Ilongo wote wakazi wa kijiji hicho.

Aidha aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na Abuu  Fadhil (22)Mzigua mkazi wa Dar Es Salaam ambaye ni tingo wa gari lililogonga Nyumba pamoja na Steven  Chiwa (26) mbembe raia na mkazi wa Nchi jirani ya Zambia ambaye ni msindikizaji wa gari hilo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala.
  
Hata hivyo wa dereva wa gari lililosababisha ajali alikimbia na gari mara baada ya tukio ambapo Kaimu Kamanda  anatoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu ya mahalialipo dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake, vinginevyo ajisalimishe mara moja.
  
Wakati huo huo  Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia  Asajile Mwamtina (46) mkazi wa kijiji cha Syukula Wilaya ya Rungwe mkoani hapa akituhumiwa kufanya mapenzi na binti yake wa miaka 13.
  
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa lilitokea juzi  majira ya saa Kumi na Mbili jioni baada ya kumvizia binti huyo (jina limehifadhiwa) ambaye aliacha shule akiwa darasa la tano mwaka 2011 kwa matatizo ya ugonjwa wa kifafa akiwa anapika.
  
Alisema mtuhumiwa alipata mwanya wa kufanya unyama huo kutokana na mkewe  ambaye  mama mzazi   wa mhanga huyo Tumikigwe Samalinga akiwa kijiji cha Kiwira kuuguza mgonjwa na kuongeza kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika.
  
Aidha katika tukio lingine eneo la Makunguru Jijini Mbeya Vyumba 12 vya biasharaa viliteketea kwa moto jana majira ya saa Tano asubuhi vilivyokuwa vimetoka kujengwa  mali ya Dominick Mbinga Mkazi wa Dar Es Salaam.


Hata hivyo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza baada ya moto huo kudhibitiwa kwa ushirikiano baina ya kikosi cha zima moto na uokoaji na wananchi.


Thamani halisi ya uhalibifu bado kujulikana pamoja na chanzo ingawa kwa mujibu wa majirani walisema inawezekana ikawa ni hitilafu ya umeme kutokana na muda huo wapangaji wa nyumba hiyo kutokuwepo wakati moto ukitokea ambao ulijulikana baada ya majirani kuona.

COLLECTION YA PICHA ZA SHOW ALIZOWAHI FANYA BEYONCE NA KUACHA ASILIMIA KUBWA YA MWILI WAKE NJE




PICHA:MADEM AMBAO WANAONGOZA KWA KUPENDWA HAPA TOWN NDIO HAWA APO




AGNES MASOGANGE
WEMA SEPETU

SNURA